Jumatano, 14 Juni 2017

ROHO MTAKATIFU - AKIPINDI CHA KWANZA

Roho Mtakatifu - kipindi cha kwanza
Pastor Lameck Stephen

Watu wengi wanamjua Roho Mtakatifu. Watu wanaosoma Biblia, wanajua mambo mengi kumhusu Roho. Jina hili hutajwa mara nyingi katika Biblia. Linatajwa katika Agano Jipya na Agano la Kale pia.
Biblia inatumia majina mbalimbali inapozungumzia Roho Mtakatifu. Sasa tunatumia jina: Roho Mtakatifu. Biblia inatumia pia majina: Roho ya Mungu, Roho, Roho ya Kristo na majina mengine pia.
Mungu alimwaga Roho yake sikukuu ya Pentekoste Yerusalemu. Na pia siku ile ile wakati wa Roho Mtakatifu ulianza. Kabla ya sikukuu ya Pentekoste ulikuwa wakati wa Baba Mungu na pia wakati wa Mwana wa Mungu, yaani wakati wa Yesu Kristo. Katika sikukuu ya Pentekoste ulianza wakati wa Roho Mtakatifu. Sasa tunaishi wakati ule.

Wakati wa Pasaka Yesu alikufa msalabani kufanya upatanisho tayari. Baada ya hayo alifufuka katika wafu akiwatokea wanafunzi wake katika siku arobaini. Aliwatokea mara chache. Kabla ya kuinuliwa mbinguni alizungumza pamoja na wanafunzi wake. Aliwaagiza wanafunzi kumngojea Roho Mtakatifu.
4. Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; 5. ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. (MDO 1:4,5)
Yesu aliwaambia: wasitoke Yerusalemu, bali waingoje Roho Mtakatifu atawajaza. Wanafunzi walifanya kama Yesu alivyowaagiza na walimngojea siku kumi. Halafu Roho alifika hapa duniani kama Yesu alivyowaahidi. Baada ya hayo Roho Mtakatifu amekaa hapa duniani kufanya kazi tangu sikukuu ya Pentekoste mpaka leo.
Kazi zake zimeendelea kama miaka elfu mbili. Wakati mwingine Roho Mtakatifu amefanya kazi pole pole. Siku hizi Mungu anawabatiza watu wengi katika Roho yake. Katika makanisa machache watu wanaojazwa na Roho wanapingwa. Wamepata karama ya Roho lakini watu wengi hawakuwaelewa wanasema kwamba ambao wamejazwa na Roho wamepotea na wamepata roho mbaya.
Pia makanisa mengi yanafundisha: "Karama za Roho Mtakatifu zilikuwa kwa ajili ya kanisa la mwanzo. Siku hizi zawadi hazifanyi kazi tena". Yanasema hivi. Lakini siyo kweli. Sisi katika kanisa la Pentekoste tunafundisha: Leo watu wanaweza kujazwa na Roho. Leo ni wakati wa Roho Mtakatifu.
Kama miaka mia moja iliyopita watu waliojazwa na Roho, walilazimishwa kuondoka kanisani. Halafu walianza kukusanyika pamoja kuomba na kuimba pamoja na baadaye walianzisha makanisa mapya. Hivi ndivyo makanisa ya Kipentekoste yalivyoanzishwa.
Siku hizi makanisa ya Kipentekoste yanakua sana duniani. Duniani kuna wa Pentekoste kama milioni mia tatu au zaidi.
Ujumbe wa Roho Mtakatifu umetokea katika makanisa mengi, siyo makanisa ya Kipentekoste tu. Kwanza kwenye makanisa ya Kipentekoste tu watu walihubiri mambo ya Roho Mtakatifu, na watu walijazwa na Roho. Lakini siku hizi katika makanisa mengi watu wanaweza kusikia mahubiri na mafundisho kuhusu Roho Mtakatifu. Katika makanisa mengi watu wanajazwa na Roho siku hizi. Na pia wahubiri wengi wanahubiri mambo ya Biblia katika Roho ya Mungu.
Roho Mtakatifu anataka kufanya kazi siku hizi sawa sawa, kama alivyofanya katika sikukuu ya Pentekoste baada ya Yesu.
Katika kipindi hiki tunasoma mambo yaliyotokea siku hiyo.
1. Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3. Kukawatokea ndimi zili zogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. (MDO 2:1-4)
Pia kabla ya siku hii watu walijazwa na Roho Mtakatifu. Ilitokea pia wakati wa Agano la Kale na wakati wa Yesu pia. Biblia inatueleza jinsi watu wengi walivyojazwa na Roho, lakini ilitokea tofauti, kuliko sikukuu ya Pentekoste na baadaye. Wakati wa Baba Mungu na wakati wa Mwana Yesu watu walipojazwa na Roho Mtakatifu, ilitokea tofauti, kama wakati wa Roho Mtakatifu, ulipoanza sikukuu ya Pentekoste. Watu walipojazwa na Roho wakati wa Mungu au wakati wa Yesu hawakusema kwa lugha nyingine. Hata Yesu hakusema kwa lugha nyingine alipojazwa na Roho baada ya ubatizo wake.
Kwa nini? Kwa sababu bado haukuwa wakati wa kusema kwa lugha. Bado haukuwa wakati wa Roho Mtakatifu. Ulianza katika sikukuu ya Pentekoste.
Wanafunzi walipojazwa na Roho, walianza kusema kwa lugha nyingine. Ilikuwa mara ya kwanza watu waliposema kwa lugha nyingine. Baada ya siku ya Pentekoste watu wengi, watu mamilioni wamesema kwa lugha mpya. Bwana asifiwe!!!!
Biblia inatueleza, kwamba Waisraeli walikuwa na sikukuu tatu kubwa Yerusalemu kila mwaka. Kila mwaka watu wengi walifika Yerusalemu wakati wa sikukuu kubwa. Sikukuu ya kwanza ilikuwa Pasaka. Ya pili ilikuwa Pentekoste. Na ya tatu ilikuwa sikukuu ya Vibanda. Sikukuu ya Vibanda ilikuwa kwa ajili ya wakati watu Waisraeli walipofika toka Misri na waliishi jangwani miaka arobaini na walikaa vibandani wakati huo.
Roho Mtakatifu alihamia duniani siku ya Pentekoste ya kwanza. Lakini siyo kamili. Mungu ni mkubwa. Yesu ni mkubwa. Roho Mtakatifu ni mkubwa, anakaa mahali pote. Biblia inasema: Lakini Mungu je! atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu… (1FAL 8:27) Lakini ni rahisi zaidi kuelewa, kama nasema: Roho Mtakatifu alihamia duniani siku ya Pentekoste.
Ndipo alianza kufanya kazi hapa duniani. Kabla ya kuhamia alikaa mbinguni, lakini sikukuu ya Pentekoste alihamia hapa. Katika sikukuu ya Pentekoste baada ya kifo cha Yesu na ufufuo wake.
Katika kipindi hiki tunasoma mambo machache kuhusu siku ya kwanza ya kazi yake hapa duniani.
Kwanza wanafunzi walijazwa na Roho Mtakatifu na walianza kusema kwa lugha nyingine. Watu wengi walisikia kama wanafunzi walivyosema kwa lugha nyingine. Kwa sababu sikukuu ya Pentekoste ilikuwa katika Yerusalemu, na ilikuwa sikukuu kubwa huko kulikuwa na watu wengi sana. Labda watu milioni moja walikuwa wamefika katika sikukuu ya Pentekoste Yerusalemu. Wanafunzi waliposema kwa lugha nyingine, sauti zao zilisikika mbali.
Pia sisi tunapoomba wakati wa kuomba ibadani tunaweza kusema kwa lugha nyingine kwa sauti.
Watu walikusanyika wengi sana. Walishangaa na walisema: “Hili ni jambo gani?” Watu wote hawakusikia kabla ya huku kusema kwa lugha nyingine.
Wanafunzi waliposema kwa lugha hawakuelewa lugha waliyosema, lakini wasikilizaji wachache waliielewa. Kwa sababu hii wasikilizaji walishangaa sana. Hawakuelewa kusema kwa lugha nyingine ni ina maana gani.
Kwanza wanafunzi walitumia karama ya lugha na watu waliwashangaa waliponena kwa lugha nyingine. Ulikuwa wakati wa kuomba katika mkutano wao na walinena kwa lugha. Baadaye ulianza wakati wa hotuba na waliacha kusema kwa lugha.
Halafu Petro alianza kuhubiri. Kwanza alisoma mistari miwili ya kitabu cha Yoeli. Mistari hii pia ipo katika kitabu cha Matendo ya Mitume, katika sura ya pili.
16. lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, 17. Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. 18. Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri. (MDO 2:16-18)
Yoeli alitabiri kwamba Mungu atamwaga Roho Mtakatifu. Na ilitokea.
Halafu Petro aliendelea kuhubiri juu ya Kristo. Aliongea kuhusu kifo cha Yesu na ufufuo wake. Na pia alikumbusha mambo machache katika Agano la Kale. Wakati huo hakukuwa na Agano Jipya. Biblia yao ilikuwa Agano la Kale tu.
Tulisoma hotuba ya Petro katika Matendo ya Mitume, sura ya pili. Lakini Biblia inatueleza ufupisho wa hotuba ya Petro. Aliongea mambo mengi zaidi.
37. Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? (MDO 2:37)
Roho Mtakatifu alifanya kazi mioyoni mwao, waliosikiliza ujumbe wa Petro. Walipomsikiliza Petro, Roho Mtakatifu aliwachoma mioyoni mwao. Wakati mwingine tunafikiri kwamba Roho anaongea na watu ambao wameokoka tu, na siyo ambao hawajaokoka. Lakini siyo kweli, Roho Mtakatifu anaongea na watu wasiookoka pia. Ndiyo kazi ya Roho hapa duniani.
7. Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 8. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 9. Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 10. kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11. kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. (YN 16:7-11)
Roho Mtakatifu anaitwa na Yesu kwa jina Msaidizi. Hapa kuna mambo mengi ambayo Roho Mtakatifu anafanya. ...atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
Roho Mtakatifu ana kazi nyingi pia siku hizi. Anafanya kazi yake katika maisha ya waaminio.
Na katika maisha ya wasioamini pia. Tulisoma katika mstari wa nane kuhusu Roho Mtakatifu: Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
Roho ananena mioyoni mwa wasiookoka kwamba mtu ni mwenye dhambi bila wokovu. Mtu amefanya mambo mengi ya dhambi. Lakini dhambi kubwa mno ni kwa sababu mtu hamwamini Yesu. Kwanza Roho anamwonyesha kwamba mtu ni mwenye dhambi na halafu anamwonyesha haki na neema. Yaani kwamba mtu anaweza kusamehewa.
Kwa kumwamini Yesu, dhambi zinasamehewa.
Roho Mtakatifu anamwonyesha hukumu pia: ... kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; (EBR 9:27)
Kila mtu atahukumiwa kadri ya matendo yake. Matendo ya watu yanaandikwa katika vitabu vya Mungu huko mbinguni. Kuna matendo mazuri na mabaya pia. Mungu atalipa mshahara kwa watu wanaofanya matendo mazuri. Kwa ajili ya matendo mabaya watu wataadhibiwa.
Watu waliookoka hawataadhibiwa kwa sababu Biblia inasema katika kitabu cha Isaya:
...Na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote. (ISA 53:6)
Yesu alipata adhabu kwa ajili ya dhambi zetu. Mungu alitoa makosa yetu na aliyaweka juu ya Yesu, Yesu alipokuwa msalabani. Yesu aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu. Si kwa ajili ya dhambi zake kwa sababu yeye hakuwa na dhambi. Lakini kwa ajili ya dhambi zetu Yesu aliangamizwa.
Kwa ajili hii tutakapofika mbele ya kiti cha enzi cha hukumu katika vitabu vya Mungu hakuna matendo yetu mabaya kwa sababu Mungu amekwisha kuyatoa na ameyaweka juu ya Yesu.
Yesu aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu.
Bwana asifiwe!
Lakini kama mtu asipomwamini Yesu, baada ya kufa kwake atapata hukumu ya milele ya Jehanamu.
Hii ni kwa sababu dhambi zinakuwa moyoni mwake na matendo yote yanamngoja katika vitabu vya Mungu. Na atahukumiwa kadri ya matendo yake.
Petro alihubiri huko Yerusalemu na Roho Mtakatifu alifanya kazi mioyoni mwa wasikilizaji. Roho alifanya kazi mioyoni mwa wasikilizaji wakati Petro alipohubiri. Hata mimi ninatumaini kwamba wakati wa mahubiri yangu Roho angefanya kazi yake mioyoni mwa watu wanaonisikiliza. Bila ya Roho Mtakatifu kazi yangu na kuhubiri kwangu ingekuwa bure kabisa.
Petro alipohubiri watu walisikia kwamba Mungu alinena nao kupitia kwa Petro.
Na hivi ndivyo kanisa la kwanza lilivyoanza. Watu waliookoka na kubatizwa walikuwa ndani ya kanisa. Sawa sawa inavyoendelea siku hizi. Kwanza lazima kuokoka na baadaye kubatizwa. Watu wa namna hiyo ni kanisa la Mungu. Watu wote wanakaribishwa kuja katika mikutano ya kanisa lakini mtu akitaka kuwa mshirika wa kanisa lazima kwanza kuokoka na kubatizwa.
Mambo mengi muhimu yalitokea katika sikukuu ya Pentekoste. Siku ile Roho Mtakatifu alianza kukaa hapa duniani na ameendelea mpaka leo. Kazi yake ilipoanza, wafuasi wa Yesu walijazwa na Roho Mtakatifu na walianza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Halafu Roho Mtakatifu alianza kufanya kazi yake ndani ya watu wasiookoka. Alifanya kazi yake wakati Petro alipohubiri.
Kazi ya Roho Mtakatifu siyo tu, kwamba watu waseme kwa lugha nyingine.
Kusema kwa lugha nyingine ni muhimu sana na tunakuhitaji.
Roho Mtakatifu anataka kufanya mambo ambayo Yesu anataka. Yesu anataka, kwamba watu wote waokoke. Na kwa ajili hii ametupa kanisa, Biblia na Roho yake. Pia kwa ajili hii ametuita kufanya kazi ya Mungu. Na Yesu anataka kwamba ambao wameokoka waweze kukua katika roho.
Roho Mtakatifu anafanya kazi pia ndani ya watu wanaomwamini Yesu.
26. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. (YN 14:26)
Yesu alitumia jina Msaidizi. Sisi tunahitaji kwamba Msaidizi atusaidie kila siku. Yesu alisema pia kwamba Roho Mtakatifu anatufundisha yote, na kutukumbusha yote ambayo Yesu ametuambia. Sasa Roho anatufundisha na kutukumbusha mambo ya Biblia. Tunaposoma Biblia au kuomba, Roho anatufundisha.
26. Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. (YN 15:26)
Tulisoma Yesu alisema: Roho wa kweli.
Tunajua kwamba Roho Mtakatifu anasema kweli.
Yesu alisema pia: yeye atanishuhudia.
Roho anamshuhudia Yesu, kwamba Yesu ni upatanisho na anatupenda.
12. Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. 13. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari. (YN 16:12-15)
Hapa tunaona mambo mengi ambayo Roho Mtakatifu anafanya katikati ya watu.
Roho anaendeleza kazi ya Yesu.
Tulisoma katika mstari wa kumi na tatu: Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote.
Makanisa yanayokubali kazi ya Roho Mtakatifu na karama zake yanalinganishwa. Roho Mtakatifu ameyaongoza. Lakini makanisa yasiyokubali Roho ni tofauti tofauti. Watu wenyewe wanajaribu kuongoza makanisa bila ya Roho ya Mungu. Lakini wanakosea.
Kwa hiyo tunamhitaji Roho Mtakatifu ayaongoze makanisa yetu, na maisha yetu pia.
Kwa sababu Mungu anatupenda alimpeleka Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu anatusaidia na kuongoza.

Mungu akubariki wewe usomaye!

by Pastor Lameck 
0757546575

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni